Categories: Africa

Kuwezesha Uvumbuzi wa Kiasilia katika Ulimwengu wa Kusini: Matarajio na Njia ya Kusonga mbele

Mozilla na Omidyar Network wanasisimka kuanzisha mpango mpya wa ulimwengu, Kuwezesha Uvumbuzi wa Kiasilia (Powering Local Innovation), ambao unalenga kuendeleza mazungumzo kuhusu “uvumbuzi wa kiasilia” katika maeneo tofauti katika Ulimwengu wa Kusini.  Mashirika washirika wetu kutoka eneo la Afrika  (AfriLabs, Lawyer’s Hub, African Union Development Agency, Thomson Reuters Foundation, Smart Africa), na kutoka India (Hasgeek), watawakutanisha pamoja wajasiriamali, wanateknolojia, watunga sera, viongozi katika sekta binafsi na wanasheria kwa mazungumzo bunifu kuhusu uvumbuzi wa teknologia inayotumika na watu, katika maeneo yao mbalimbali,  hivi sasa na itakayotumika katika siku za baadaye.

Mpango huu unakusudia kusaidia mbinu mpya za uvumbuzi wa kiasilia zinazowezesha na kuhusisha wadau wa Kiafrika. Mwaka uliopita, tuliunga mkono hafla iliyoandaliwa na Lawyer’s Hub, yenye mada Mtaji Mweupe, Wakurugenzi Weusi (“White Capital, Black Founders”). Hafla hii ilihoji jinsi upendeleo wa mbari, utaifa na wa kitabaka unavyowekea mipaka fursa zinazoletwa na makampuni na wawekezaji wa kigeni  kwa wavumbuzi wa Kiafrika. Halfla hii ilifuatiwa na utafiti wa Afrika yote uliofanywa na Afrilabs kuelewa chamgamoto muhimu zinazowakabili wajasiriamali wa kiteknologia, kama upatikanaji wa mtaji, vizuizi vya kisheria na sera, ushirikiano wa kuvuka mipaka ya nchi, na ushindani unaohusiana na majukwaa yaliyodhibitiwa mtandaoni. Wakati huo huo, wasimamizi wa India wameongeza shughuli za kisera zinazolenga kukuza ‘mabingwa wa kitaifa’ na vile vile kukuza wazo la mfumo wa ikolojia ya mtumiaji wa India la “kujitegemea” kama ushindani kwa  utawala wa soko la Silicon Valley. Haswa, wimbi hili la sera limepokea upinzani kutoka kwa asasi za kiraia na sehemu za jamii ya waanzilishi wa biashara ambao wanahoji kuwa hatua hizi zinaweza kusababisha nguvu kukita mizizi miongoni mwa wanabiashara wachache nchini, na hivyo kuendeleza changamoto zinazohusishwa na mbinu za kibiashara za Silicon Valley.

Kuendeleza mradi wa Mozilla wa Kubuni Tena Maana ya Wazi(Mozilla’s Reimagine Open), mpango wa Kuwezesha Uvumbuzi wa Kiasilia utachunguza kama na jinsi kanuni za msingi za uwazi zinaweza kutumika kwa mifumo ya uvumbuzi katika Ulimwengu wa Kusini. Mitchell Baker, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mozilla, ametetea kwamba wazo la “wazi” halipaswi kuchaguliwa na mifumo na kampuni ambazo hazizingatii kanuni za ufikiaji, uwezeshaji, na fursa ambayo ilifanya mtandao wazi wa asili kufanikiwa.

Katika kipindi cha miaka miwili ijayo, washirika wetu watatekeleza shughuli zinazolengwa kimkoa  ambazo zinajenga juu ya nguvu zao za shirika. Shughuli hizi zitajumuisha safu ya majadiliano ya baadhi ya washika dau, hackathons za sera, nakala za habari, utafiti na warsha zinazolenga kushughulikia changamoto kuu zinazokabili biashara ndogo sana, biashara ndogo, za kati na mifumo ya waanzilishi wa biashara katika eneo za Afrika na India na kupendekeza suluhisho. Shughuli hizi zitaendeleza malengo ya kipekee ya Mradi wa Ubunifu wa Afrika(Africa Innovation Mradi), kunufaika na jukumu la Mozilla kama msimamizi wa wavuti wazi kukuza mifano ya uvumbuzi ambao umezingatia mahitaji ya kipekee ya watumiaji katika bara la Afrika na India.

Kile washirika wetu wanasema kuhusu mpango wa Kuwezesha Uvumbuzi wa Kiasilia:

AfriLabs

Hapa Afrilabs tunaaminia nguvu ya wavumbuzi na wajasiriamali kukuzia suluhisho changamoto kubwa katika jamii zao. Kama ekolojia ya bara ya vituo 292 katika nchi 49 za Afrika, tunafanya kazi kuhakikisha kuwa fursa, ufadhili, zana za uvumbuzi na ustadi wa kiufundi zinapatikana kwa wavumbuzi hawa kote barani bila kuzingatia jinsia, umri, eneo, lugha na sababu zingine.  Tunafurahi kufanya kazi na Mozilla, Omidyar, na washiriki wa jamii yetu kuwezesha uvumbuzi wa kiasilia na kuchochea suluhisho zenye uwezo wa kukua na kuenea, zenye ujasiri na zinazojumuisha zilizo na mizizi barani Afrika.

AUDA-NEPAD

African Union Development Agency – AUDA-NEPAD inafurahi kushirikiana na washirika anuwai kwenye mpango huu ambao utachangia uvumbuzi wa kienyeji kote barani. Kukuza uwazi na mazungumzo ya wazi ili kuboresha mfumo wa ikolojia wa uvumbuzi humu Afrika ni muhimu kuelekea kufikia Afrika Tunayotaka(the Africa We Want) kama ilivyoagizwa katika Ajenda ya AU 2063″.

Hasgeek

Hasgeek inakuza mazungumzo kati ya wataalamu wa teknolojia ili kuhimiza kuenea kwa maoni mazuri na kuendeleza mazingira kwa ujumla. Hasgeek ni mbia katika mpango wa Kuwezesha Uvumbuzi wa Kiasili katika Ulimwengu wa Kusini ili kukuza umakinifu wa fikra kuhusu jukumu la programu zenye chanzo wazi katika uvumbizi nchini India na changamoto ambazo zinakabili biashara ndogo na za kati kwa kuzingatia kukubali na kutumia programu zenye chanzo wazi na kunufaika kwa kutumia programu zenye chanzo wazi kwa uvumbuzi. Hasgeek itaangalia tajriba za kienyeji kutoka kwa taswira ya weledi.

Lawyers Hub

Lawyers Hub ilianzishwa kutumikia Afrika kwenye sera za kidijitali na uvumbuzi wa haki kwa kutoa sera mpya za kuvumbua na suluhisho zinazoendeshwa na teknolojia. Kwa hivyo tunafurahi kushiriki katika ari ya Kuwezesha Uvumbuzi wa Kiasilia katika Ulimwengu wa Kusini wa Mozilla kwani uvumbuzi wazi na wa kiasilia ni chombo muhimu kwa maendeleo ya mazungumzo ya sera za kiasilia juu ya maswala yanayoibuka na ya kimfumo. Mradi huu utaelekeza mazingira yenye sera dhabiti za uvumbuzi, kukuza mtandao wenye afya bora zaidi na kulinda haki za kidijitali katika eneo la Afrika.

Omidyar Network

Ufadhili wa Omidyar Network kwa kazi hii ulihusisha kusaidia asasi za kiraia barani Afrika, na waandishi wa habari wanaojitegemea, ili kuimarisha sera na muundo wa teknologia ya sera nyingi za uvumbuzi wa teknologia ambazo zinawasilishwa na serikali za Afrika. Kazi hii inasaidia na kupanua jalada letu inayolenga kuimarisha kanuni katika uchumi wa kidijitali, kuboresha ushawishi wa taasisi za kiafrika kwa teknolojia inayoibuka na kufuatilia juhudi za mabadiliko ya tarakimu barani Afrika.

Thomson Reuters Foundation

“Tunafurahi kushirikiana na Mozilla na Omidyar Network katika mpango huu wa maana. Tunaongozwa na kanuni zetu za uaminifu; hizi ni usahihi, uadilifu na uhuru wa kutopendelea upande, tutatumia nguvu ya uandishi wetu wa habari na wa kutangaza, kuangazia maswala yasiyoripotiwa – na yasiyoeleweka – ya uvumbuzi na haki za kidijitali katika bara la Afrika.” alisema  Antonio Zappulla, Mkurugenzi Mtendaji wa Thomson Reuters Foundation.

Kuhusu Mradi wa Uvumbuzi Afrika

Mpango wa Kuwezesha Uvumbuzi wa Kiasilia Afrika ni Mradi wa Uvumbuzi Afrika wa Mozilla, mpango ambao unataka kukuza mazingira ya washirika wanaofanya kazi kuendeleza mtandao wenye afya bora zaidi na kukuza uvumbuzi unaotokana na mahitaji ya kipekee ya watumiaji katika eneo la Afrika

Ili kujua zaidi au kama una maswali, tafadhali wasiliana na Noémie Hailu, Meneja wa Programu, Africa Innovation Mradi, nhailu@mozilla.com.

Mozilla: www.mozilla.org